25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

CUF kurejesha ofisi zao zilizochukuliwa na ACT Wazalendo

BEATRICE KAIZA -DAR ES SALAAM

Chama cha Wananchi CUF kimesema kuwa kimeazimia kurejesha ofisi zake zote zilizochukuliwa na chama cha ACT Wazalendo hususan Visiwani Zanzibar.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaama na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho, Mussa Haji Kombo, ambaye alisema kuwa ofisi hizo ni mali ya CUF hivyo ni lazima wazirejeshe.

“Kwa kuwa baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF limeazimia kurejesha ofisi  zake zilizoporwa na ACT kupitia kikao chake cha hivi karibuni sisi viongozi tutazirejesha na tupo tayari kwa lolote na wala hatuna hofu na vitisho vya Maalim Seif na wafuasi wake.

“Ikumbukwe kuwa ofisis hizi ni za chama chetu, tunaendelea na nutaratibu wa kuzirejesha na aSerikali iache kukuablia vitisho vya mtu mwenye ubinafsi kupindukia na asiejali umpoja na mshikamano wa Taifa letu,” alisema Kombo.

Katika hatua nyingine, Kombo alimtuhumu Maalim Seif kuwa ni mbaguzi na mwenye kupandikiza chuki miongoni mwa jamii ya watanzania.

“Unaweeza kuona tu kuwa mtu huyu amekuwa chanzo cha kufarakana kwetu kupitia hoja zake mbalimbali zikiwamo zile za ubara na uzaznzibar hiki ni kielelezo cha uchovu wa fikra zake.

“Hivi kila ahamae chama ataondoka na alichoingia nacho au alichochangia chamani kwani Hajji Duni alipohamia chadema aliondoka na kitu? Au wabunge wa Cahdema na Cuf walipojiunga na CCM waliondoka na ofisi zao? Hivyo mlazima tufakari upya jambo hili na tulipinge kwa nguvu zote,” alisema.

Upande wake Mkurugenzi wa Haki za Binadamu wa Chama hicho, Haroub Mohamed Shamis, amesema kuwa chama hicho kimechoka kugombwanishwa na kufitinishwa kwa maslahi ya mtu mmoja hivyo sasa kimerejea kwenye misingi yake kama ilivyokuwa dhumuni la kuundwa kwake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles