21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

CROATIA KUMKOSA VRSALJKO

MOSCOW, URUSI


TIMU ya taifa ya Croatia inatarajia kumkosa beki wa kulia, Sime Vrsaljko,  katika mchezo wa kesho dhidi ya England kutokana na maumivu makali ya kifundo cha mguu.

Beki huyo aliumia katika mchezo uliopita dhidi ya Urusi ambao Croatia ilipenya kwa mikwaju ya penalti 4-3  baada ya dakika 90 kumalizika zikifungana mabao 2-2.

Beki huyo anayecheza katika timu ya Atletico Madrid, alipumzishwa katika mchezo dhidi ya Urusi dakika ya 90 na inadaiwa kuwa hatakuwapo katika mchezo dhidi ya England.

Beki huyo alicheza michezo yote ya michuano ya Kombe la Dunia tangu ilipoanza Juni 14, mwaka huu nchini Urusi, kasoro mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Iceland.

Nafasi ya beki huyo ilichukuliwa na Domagoj Vida, katika mchezo dhidi ya Urusi hata hivyo katika mchezo dhidi ya England nyota wa Bayer Leverkusen,  Tin Jedvaj, anatarajia kuchukua nafasi hiyo.

Wakati huo huo kuna wasiwasi kuhusu afya ya kipa wa timu hiyo, Danijel Subasic, ambaye alionekana  kuumia katika mchezo dhidi ya Urusi.

Upande wa England wanatarajia kumkosa Jordan Henderson, kutokana na kusumbuliwa na msuli na maumivu ya  msuli wa paja aliyopata katika mchezo wao na Sweden.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles