23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Cristiano Ronaldo ajiunga kikosini Juventus

 TURIN, ITALIA 

KWA mujibu wa taarifa kutoka ndani ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Italia, Juventus, wamedai kuwa staa wao Cristiano Ronaldo alitakiwa kuripoti kikosini jana kwa ajili ya kujiunga na wachezaji wenzake. 

Mchezaji huyo alikuwa nyumbani kwake nchini Ureno kwa ajili ya kujikinga na virusi vya corona tangu Machi mwaka huu, lakini uongozi wa timu yake umewataka wachezaji wote wa kigeni kujiunga na kikosi hicho kwa ajili ya maandalizi ya kumalizia msimu huu. 

Ronaldo alikuwa mmoja kati ya wachezaji wa kigeni ambao waliruhusiwa kurudi kwao, hivyo jana mchezaji huyo alikuwa anasubiriwa kwenye kiwanja cha ndege. 

Hata hivyo mchezaji huyo baada ya kuwasili nchini Italia atatakiwa kukaa karantini kwa wiki mbili kwa ajili ya kuangaliwa kama atakuwa na maambukizi yoyote ya virusi hivyo vya corona, hivyo Ronaldo ataungana na wachezaji wenzake katikati ya Mei. 

Waziri mkuu nchini Italia, Giuseppe Conte, ameliwashia taa ya kijani shirikisho la soka nchini humo kuendelea na ratiba zao huku wakizitaka timu kuanza kufanya mazoezi Mei 4 mwaka huu kwa ajili ya kujiandaa na kumalizia msimu huu. 

“Tunaamini ligi itaendelea kama kawaida endapo mambo yatakwenda vizuri, tunajua kila kitu kitakuwa sawa siku za hivi karibuni,” alisema waziri huyo. 

Italia ni moja kati ya taifa ambalo limeathirika kwa kiasi kikubwa na virusi vya corona tangu vilipogundulika Desemba mwaka jana huko nchini China. 

Hadi sasa Italia ina jumla ya maambukizi ya watu 199,414, huku jumla ya watu 26,977 wakipoteza maisha na wengine 66,624 wakipona. Kwa sasa wanapambana kuhakikisha wanazuia maambukizi mapya. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,426FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles