30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Cristiano Ronaldo afikisha mabao 500

Football/Soccer: Spanish "Super Cup" - Atletico de Madrid vs Real MadridMADRID, HISPANIA

NYOTA wa timu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amefanikiwa kufikisha mabao 500 katika historia yake ya soka baada ya juzi kuifungia klabu yake mabao mawili katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Malmo.

Mabao hayo ya Ronaldo yametokana na kucheza michezo 753 katika klabu mbalimbali pamoja na timu yake ya taifa ya Ureno.

Hata hivyo, amekuwa ni mchezaji ambaye anaongoza kwa mabao mengi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa, huku akiwa na jumla ya mabao 82, akimuacha mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi, mabao matano ambaye ana mabao 77.

Baada ya kufikisha mabao hayo, Ronaldo amefanikiwa kuongea na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza tangu miezi tano iliyopita kutokana na kushambuliwa na waandishi wa habari, lakini baada ya mchezo wa juzi alifanikiwa kuongea.

“Ni furaha kuisaidia timu yangu kufanya vizuri, ninaamini nitaendelea kufanya hivyo kwa kuwa bado nina nafasi, nilikuwa kimya sana kuongea na vyombo vya habari kutokana na maswali yao yanakuwa si mazuri, wanaweza kukuuliza swali kutokana na tukio ambalo lilifanyika miezi sita iliyopita,” alisema Ronaldo.

Hata hivyo, kutokana na mabao hayo, Ronaldo ameifikia rekodi ambayo iliwekwa na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Raul Gonzalez, ambaye alipachika mabao 323 akiwa na klabu hiyo baada ya kucheza michezo 741 kuanzia mwaka 1994 hadi 2010, huku Ronaldo akicheza michezo 308 na kuifikia rekodi hiyo.

“Furaha nyingine ambayo ninayo ni kuifikia rekodi ambayo iliwekwa na Raul, lakini kitu muhimu zaidi ni kuibuka na ushindi na klabu yangu kwa kuwa mchezo ulikuwa mgumu,” aliongeza Ronaldo.

Ronaldo, mwenye umri wa miaka 30, alijiunga na klabu ya Real Madrid mwaka 2009, akitokea Manchester United na amefanikiwa kuchukua uchezaji bora wa dunia wa Ballon d’Or msimu uliopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,195FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles