26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

CRDB yawapa zawadi za kufunga mwaka wanafunzi vyuoni

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Benki ya CRDB imetoa zawadi kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu ya kampeni ya JIPE 5 ambayo ilizinduliwa Oktoba mwaka huu ikilenga kuhamasisha Watanzania kujiwekea akiba kuelekea mwisho wa mwaka.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Meneja Mwandamizi wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Abel Lasway, amesema hadi kufikia leo Desemba 16, benki tayari imeshatoa zawadi zinazofikia Sh milioni 20.

Zawadi hizo zimetolewa kwa wateja zaidi ya 4000 huku akaunti zaidi ya 74,000 zikiwa zimekwisha funguliwa.

“Tunawashukuru sana Watanzania kwa kuipokea vyema kampeni ya Jipe Tano ambapo mafanikio yaliyopatikana sio tu ni kwa faida ya Benki ya CRDB bali yanaonyesha ni kwa jinsi gani benki imeweza kuwajumuisha Watanzania wengi katika mfumo rasmi wa huduma za fedha,” amesema Lasway.

Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Abel Lasway (katikati) akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa kampeni ya JIPE 5 na Scholar ambayo inaendeshwa na benki hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo hapa nchini. Kulia ni Meneja wa Udhamini na Matukio wa Benki ya CRDB, Lilian Kanora na kushoto ni Evance Mkao ambaye ni Meneja Uhusiano Upande wa Mauzo.

Meneja huyo amesema katika kampeni hiyo ya Jipe Tano makundi mbalimbali ya wateja yameweza kuzawadiwa ambapo kwa mwezi huu benki inawazawadia ada za shule wazazi wanaofungua akaunti ya watoto ya Junior Jumbo ambapo Sh milioni 30 zimeandaliwa.

“Benki ya CRDB tunajinasibu kwa kaulimbiu yetu ya ‘Ulipo Tupo’ ambayo haiishii tu kufikisha huduma mahali ambapo wateja wetu wapo bali inalenga kuhakikisha benki inakua pamoja na mteja katika hatua zote za maisha yake,” amesema.

Amesema pia Benki ya CRDB ililenga kundi la wanafunzi wa vyuo ambavyo vimefunguliwa hivi karibuni ambapo timu ya mauzo ya benki iliweka kambi katika vyuo mbalimbali nchini ili kutoa elimu ya masuala ya fedha pamoja na kutoa huduma za kufungua akaunti kwa wanafunzi.

“Nimefurahi kuona tumeweza kufanikiwa kuwaingiza katika mfumo rasmi wa fedha wanafunzi wengi na tukaona pamoja na kuwapa huduma hizi tuweze kuwazawadia vitu ambavyo vitarahisha maisha yao wawapo chuoni,” amesema Lasway.

Aidha amesema kupitia kampeni hiyo ya wanafunzi ya JIPE 5 na Scholar, jumla ya wanafunzi 100 kutoka vyuo mbalimbali nchini watazawadiwa laptop (kompyuta mpakato) na smart phone (simu janja).

Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa laptop, Jackline Masayanyika mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino kilichopo jijini Mwanza, amesema zawadi hiyo itakuwa msaada mkubwa katika masomo yake hasa kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za masomo zinazopatikana mtandaoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles