23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

CRDB yawadhamini wajasiriamali 58

Na GUSTAPHU HAULE-PWANI

BENKI ya CRDB, imewadhamini zaidi ya wajasiriamali wanawake 58 waliopo katika kikundi cha Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Mkoa wa Pwani, ili waweze kushiriki maonyesho ya bidhaa za viwandani yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Sabasaba, vilivyoko Kibaha Picha ya Ndege, Mkoa wa Pwani.

Meneja wa CRDB Kibaha, Rosemary Nchimbi, aliyasema hayo juzi, wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali, wakiwamo Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, Waziri wa Nishati. Dk. Medard Kalemani na wananchi mbalimbali waliokuwa wametembelea maonyesho hayo.

Nchimbi, alisema kuwa, CRDB iliamua kuwadhamini wajasiriamali hao ili waweze kupata fursa ya kushiriki maonyesho hayo na kutangaza bidhaa zinazotengenezwa kupitia vikundi vyao.

“Benki yetu iliamua kujitolea bure kuwasaidia wanawake hao na itaendelea kuwadhamini miaka mitatu mfululizo ili kuhakikisha na wao wanafaidika na maonyesho ya bidhaa za viwandani yanayofanyika  mkoani Pwani na hata katika maeneo mengine nchini,” alisema Nchimbi.

Pamoja na hayo, Nchimbi aliwataka wajasiriamali ambao wapo nje ya vikundi, kuhakikisha wanajiunga kwa haraka kwenye vikundi ili waweze kufaidika na fursa za mikopo na pamoja na udhamini mwingine unaotolewa na CRDB.

Kwa mujibu wa Nchimbi, kitendo cha baadhi ya wajasiriamali kuwa nje ya vikundi kinawafanya wasipate baadhi ya huduma zinazotolewa na taasisi za fedha, ikiwamo Benki ya CRDB.

“CRDB tuliona ni vema tukawashirikisha wajasiriamali wanawake wa Mkoa wa Pwani kushiriki maonyesho hayo kwa kuwalipia gharama zote, japokuwa hawakuwa wateja wetu.

“Pamoja na hayo, tutaendelea kuwadhamini miaka mitatu mfululizo, ili nao waweze kutambulika na kuweza kupata masoko ya kuuzia bidhaa zao kirahisi,” alisema Nchimbi.

Kwa upande wake, Katibu wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi, Mkoa wa Pwani, Elina Mgonja, aliishukuru benki hiyo kwa hatua kubwa waliyofanya katika kuwadhamini wajasiriamali hao kwa kuwa imewasaidia kutangaza bidhaa zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles