24.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 2, 2024

Contact us: [email protected]

CRDB yapongezwa kwa kuinua Wanawake kiuchumi

Na Allan Vicent, Tabora

Benki ya CRDB imepongezwa kwa kuanzisha huduma mbalimbali za uwezeshaji  makundi ya kijamii jambo ambalo limewezesha wanawake wajasirimali walio wengi kunufaika kiuchumi.

Pongezi hizo zimetolewa juzi na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Tabora, Safia Jongo alipokuwa akiongea katika kongamano la wanawake wajasiriamali lililoandaliwa na benki hiyo katika kuadhimisha siku ya Malkia wa CRDB.

Baadhi ya akinamama wajasiriamali Mkoani Tabora wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani humo ACP Safia Jongo katika Kongamano la Huduma ya Malkia wa Benki ya CRDB lililofanyika hivi karibuni Mkoani humo. Picha na Allan Vicent. 

Alisema kuwa wanawake ndio msingi wa mafanikio ya familia na jamii kwa ujumla, hivyo wakiwezeshwa wana uwezo wa kufanya mambo makubwa kupitia shughuli zao.

Alibainisha kuwa asilimia 80 ya wanawake wanaojishulisha na biashara hutumia huduma za kibenki kwa kuweka akiba na kukopa lakini wengi wao hushindwa kuendelea kutokana na riba kubwa wanazotozwa na taasisi za fedha zisizo rasmi.

“Naipongeza benki ya CRDB kwa kujali wanawake na kuanzisha huduma rafiki kwa lengo la kuwainua kiuchumi, ni dhahiri ukimwezesha Mwanamke umeinua familia yake na jamii inayomzunguka,” amesema Safia.

Kamanda Safia alifafanua kuwa taasisi zisizo rasmi zimekuwa zikiwarudisha nyuma kimaendeleo akinamama wanaokopa kwao kwa kuwatoza riba kubwa jambo ambalo hupelekea kushindwa kuinuka kiuchimi.

Alisisitiza kuwa benki ya CRDB ni mfano wa kuigwa kwa taasisi nyingine za kifedha kwani huduma zao zimekuwa zikijikita kumuinua mwanamke na sio kumgandamiza ikiwemo kuwapunguzia riba ya mikopo wanayochukua.

Aidha aliipongeza benki hiyo kwa kubuni bidhaa rafiki zinazoendana na mahitaji ya wanawake nchini huku lengo kuu likiwa kuwawezesha kufanya mambo makubwa ili kujiongezea kipato na hatimaye kuinuka zaidi kiuchumi.

Safia alibainisha kuwa bidhaa ya malaika ambayo ni mahususi kwa wanawake ni muhimu sana kwani itawawezesha kufikia ndoto zao hivyo akatoa wito kwa wanawake kuchangamkia huduma hiyo na nyinginezo zinazotolewa.

Awali Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Magharibi, Said Pamui alisema kuwa beki hiyo imekuja na suluhu ya changamoto zote wanazokumbana nazo wanawake ambapo itahakikisha mikopo yote inakuwa na riba ndogo na kupewa elimu.

Alibainisha kuwa lengo ni kuhakikisha huduma zote zinazoanzishwa na benki hiyo zinawanufaisha wateja wao wote na hakuna usumbufu wowote katika bidhaa hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles