23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

CRDB: Tumetoa Bilioni 100 kwa wanunuzi wa pamba

Derick Milton, Simiyu

Benki ya CRDB imesema katika kipindi cha mwaka huu cha ununuzi wa zao la pamba nchini mpaka sasa imetoa kiasi cha zaidi ya Sh. Bilioni 100 kwa wanunuzi wa pamba nchini.

Benki hiyo imesema licha ya zao hilo kukumbwa na changamoto ya bei katika soko la duniani, imeendelea kuwasaidia wanunuzi ili waweze kununua pamba yote iliyopo kwa wakulima.

Kauli hiyo imetolewa Kaimu Mkurugenzi wateja wakubwa wa Benki hiyo, Prosper Nambaya kwenye ziara ya mwekezaji kutoka nchini Uturuki Mustafa Albayram na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Prof. Elizabert Kiondo mkoani Simiyu ya kuangalia eneo la uwekezaji wa kiwanda kikubwa cha nguo.  

Nambaya amesema benki hiyo itaendelea kusaidia sekta ya kilimo hasa kwenye zao la pamba, ambapo hatua za awali wamewezesha kupatikana kwa mwekezaji huyo kutoka nchini Uturuki ambaye atajenga kiwanda kikubwa cha nguo mkoani Simiyu.

“Baada ya kuona pamba imepata changamoto ya bei katika msimu wa mwaka huu, kama benki tuliamua kwenda nchini Uturuki na kuongea na Balozi wetu Prof. Kiondo ambaye alitusaidia kuongea na wanunuzi wakubwa wa Uturuki.

 “Haya matunda ambayo tunayaona hapa leo ni jitihada za benki yetu katika kuhakikisha zao la pamba na wakulima wake hawapati changamaoto tena ya bei kama ilivyokuwa mwaka huu, tumefanikiwa kumleta mwekezaji huyu ambaye atajenga kiwanda hapa Simiyu,” amesema Nambaya.

Aidha amesema kuwa beki hiyo ipo tayari kutoa msaada wowote wa kifedha kwa mwekezaji huyo katika hatua za awali mpaka kiwanda kinajengwa na kuanza kufanya kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles