Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital
Benki ya CRDB imesaini mkataba wa makubaliano ya kuwawezesha wafanya biashara wanaoagiza mizigo kutoka nje ya nchi kupitia kampuni ya Silent Ocean, kuwawezesha kupata mzigo yao kwa wakati.
Akizungumza na waandishi wa habari Machi 21, 2023 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul amesema kuwa wameingia makubaliano ya kuwawezesha wafanyabiashara ambao wanaagiza bidhaa kutoka nje na nchi.
“Tumeshirikiana na Silent Ocean kuongeza wigo kwa wafanyabiashara wanaosafirisha mizigow bandarini na kuleta unafuu wa kukomboa mizigo yao.
Makubaliano haya ni kuwawezesha wafanyabiashara ambao wanaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kupitia Kampuni ya Silent Ocean tukishirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Silent Ocean, Salaah Mohamed,” amesema Bonaventure.
Ameongezea kuwa ili waweze kukidhi mahitaji ya siko na wakati huo huo kuepuka gharama za ziada zinazotokana na mzigo kukaa muda mrefu bandarini, ambapo wafanyabiashara hao watawezeshwa mkopo wa riba nafuu kwa kipindi cha miezi sita.
Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Benki ya CRDB, Mussa Lwila amesema kuwa makubaliano hao ya kuwawezesha wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kupitia kampuni ya silent Ocean ili waweze kukidhi mahitaji ya soko na wakati huo watawezeshwa mkopo wa riba nafuu kwa kipindi cha kuanzia mwezi mmoja hadi miezi sita.