26.1 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

CRB yaonya kazi zisizo viwango

NA FLORENCE SANAWA -MTWARA

MSAJILI wa Bodi ya Wakandarasi (CRB), Rhoben Nkori amewaonya wakandarasi wadogo wanaofanya kazi zisizo na viwango kufuata mikataba ya miradi inavyosema ili kupunguza malalamiko.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya usimamizi wa mikataba ya ujenzi kwa makandarasi wa mikoa ya Lindi, Mtwara na maeneo mengine jana, alisema hali hiyo haikubaliki.

Nkori alisema wakandarasi wadogo wamekuwa wakifanya kazi zisizo na viwango hali ambayo inasababisha kuwapo makelele dhidi yao. 

Alisema wakandarasi hawako makini katika utekelezaji wa majukumu yao hali ambayo inachangia kushindwa kusimamia vizuri mikataba wanayoingia.

Nkori alisema lawama nyingi zimekuwa zikitolewa kwa wakandarasi wadogo kwa kuwa hawako makini kusimamia na kutekeleza mikataba yao ya kazi hali ambayo inachangia kukosekana imani kwao. 

“Unajua ifikie wakati tuelezane ukweli ili tujirekebishe, inawezekanaje upewe kazi kama mkandarasi alafu ushindwe kuisimamia na kuruhusu kulaumiwa? Hasa hawa wakandarasi wadogo.

“Ukiangalia hali halisi, hii mikataba ya ndani makandarasi wamekuwa wakilaumiwa, tumejifunza wengi hawako makini kusimamia mikataba.

“Bodi ina kazi kubwa ya kuwakumbusha ili mfanye kazi inayotakiwa bila kuwapo na ubabaishaji wa aina yoyote ndiyo maana tunapiga kelele tunataka mbadilike…,” alisema Nkori.

Mshiriki kutoka mkoani Mtwara, mhandisi Engeltraud Mbemba aliitaka Serikali iwasaidie kupitia bodi kupunguza  gharama za ada ya usajili kwenye halmashauri zao.

“Hawa wakandarasi wanalipa ada kubwa, tunaomba Serikali kupitia Bodi ya Wakandarasi kuliona hili na kuwasaidia kwakuwa wanalipa Sh 300,000 kwa mwaka kwa daraja la 7, hii ni kubwa kulingana na daraja walilopo,” alisema Mpemba.

Mhandisi Henry Shimo alisema mbali na kazi zinazofanywa na bodi hiyo, anaomba kutolewa taarifa ya mrejesho wa uhakiki wa makandarasi maeneo mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles