24.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Countbouy ajitabiria makubwa chini ya Pace Vent Label

Accra, Ghana

Msanii anayekuja kwa kasi kutoka Ghana, Mustapha Kwaku Kumasah maarufu kama, Countbouy Muss, ameweka wazi ndoto zake kulipaisha bara la Afrika chini Pace Vent Label.

Countbouy Muss, amesema alianza sanaa akiwa shule ya St Dominic Junior High School na baadaye sekondari ya Suhum Senior High School Technical.

“Nimezaliwa huko Koforidua Mashariki mwa Ghana na toka kipindi hicho nilianza kupenda muziki. Sasa hivi nasoma Shahada ya Usimamizi wa Biashara katika chuo cha Ghana Technology University College. Nikiwa sekondari nilionekana kwenye TV Taifa wakati wa sikukuu ya shule nikiimba na kusoma hotuba mwaka 2012 na 2017 niliachia kazi mbili ambazo ni Loose Control na STM kabla sijaanza kufanya kazi na Pace Vent Label nikiwa kama msanii na msimamizi wa lebo.

“Mimi bado ni msanii mchanga mwenye ndoto za kuiweka Afrika kwenye ramani ya dunia, naweza kuimba, kurap, kuweka melodi kwenye viitikio na kunogesha nyimbo,” ameesema Countbouy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,268FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles