23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

COSTA: KWAHERINI CHELSEA, SINA TATIZO NA CONTE

SAO PAULO, BRAZIL

BAADA ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England, Chelsea, kufikia makubaliano na klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania juu ya kuwauzia mchezaji wao wa zamani, Diego Costa, mchezaji huyo amefunguka na kusema hana tatizo na kocha wake, Antonio Conte.

Kocha huyo baada ya kuchukua ubingwa wa ligi msimu uliopita na wachezaji wakiwa kwenye mapumziko nchini kwao, alimtumia ujumbe wa maandishi mchezaji huyo ambaye alikuwa anaongoza kwa mabao ndani ya Chelsea na kumwambia kwamba hayupo kwenye mipango yake katika msimu wa 2017/18.

Kutokana na hali hiyo, Costa hakuweza kurudi kikosini japokuwa kuna wakati uongozi ulikuwa unamhitaji, ila aliweka wazi kuwa hana mpango wa kurudi na mikakati yake ni kuhakikisha anajiunga na klabu yake ya zamani na Atletico Madrid.

Costa alijiunga na Chelsea mwaka 2014 akitokea Atletico Madrid kwa uhamisho wa pauni milioni 32, lakini kwa sasa anarudi Atletico Madrid baada ya kukubaliana kwa kitita cha pauni milioni 60.

Tayari mchezaji huyo amewasili nchini Hispania kwa ajili ya kumalizana na Atletico ndani ya saa 48 kuanzia sasa baada ya kukamilisha vipimo vyake.

“Ninaamini kila kitu kipo sawa ndani ya klabu ya Chelsea, sina tatizo na mchezaji yeyote ndani ya klabu hiyo wala kocha Antonio Conte ambaye alinitumia ujumbe wa kwamba hanitaki kwenye kikosi chake.

“Hata kama kuna mtu ambaye nilikwaruzana naye, lakini nadhani kila kitu kilikuwa sawa baada ya muda, hivyo ninaondoka kwa amani bila tatizo na mtu yeyote,” alisema Costa.

Costa mwenye umri wa miaka 28, anatarajia kumalizana na Atletico Madrid mapema wiki ijayo, lakini hataweza kucheza hadi Januari kutokana na klabu hiyo kufungiwa kusajili wachezaji kwa mwaka mmoja ambapo adhabu yake itamalizika Januari mwakani.

Mshambuliaji huyo ataendelea kuchukua kiasi cha pauni 150,000 kwa wiki, ambazo ni zaidi ya milioni 452, kiasi ambacho kinalingana na kile alichokuwa anachukua katika klabu ya Chelsea msimu uliopita.

Akiwa katika klabu ya Chelsea, alifanikiwa kupachika jumla ya mabao 59 kwa michezo 120 aliyocheza na kutwaa taji la Ligi Kuu England mara mbili na Kombe la Ligi mara moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles