27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

COSOTA yakamata wazalishaji 11 wa kazi za wasanii

Na Anitha Jonas-COSOTA, Dar es Salaam

Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) imefanya operesheni katika baadhi ya maeneo ya uzalishaji wa kazi za Filamu na Muziki na ambapo kukamata zaidi ya mashine 50 zenye uwezo wa kudurufu takribani nakala 10,000 kwa nusu saa.

Operesheni hiyo ya uharamia wa kazi za muziki na filamu imefanyika Mei 18, 2021 Kariakoo, Jijini Dar es Salaam ambapo takribani watuhumiwa kumi na moja wanafanya shughuli za uazalishaji wa kazi haramu za filamu na Muziki walikamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi Msimbazi kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.

Akizungumza katika Operesheni hiyo Mwanasheria wa COSOTA, Lupakisyo Mwambinga alieleza kuwa suala uharamia wa kazi za Muziki na Filamu umekithiri nchini hivyo COSOTA imedhamiria kukomesha hilo kwa kufanya operesheni endelevu za kukamata kazi zote nje na ndani ambazo zinazalishwa bila kufuata sheria.

“Kifungu cha 42 cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki kamakilivyofanyiwa marekebisho na Sheria namba 3 ya mwaka 2019 kinasema ukikamatwa kwa kosa la uvunjifu wa Hakimiliki faini yake ni isiyopungua milioni ishirini au Kifungo cha Miezi sita na kisichozidi Miaka Mitatu au vyote kwa pamoja,”alisema Mwambinga.

Pamoja hayo Mwanasheria huyo alitoa onyo kali kwa wazalishaji wote na wasambazaji wa kazi za Muziki na Filamu ambao wanaburn CD za Muziki na Filamu, wanaoweka Muziki kwenye flash kwa kusema kuwa hilo ni kosa, na alisisitiza kuwa COSOTA imedhamiria tutahakikisha tunathibiti hilo na kwa yoyote atakayekamatwa na kazi hizo zisizo na mikataba au makubaliano na wamiliki atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Pia Mwambinga alifafanua kuhusu udurufu wa Filamu za nje bila kufuata utaratibu kuwa ni kosa na aliwasihi wazalishaji hao  kuachakudanganyana, kwa kusema udurufu au uzalishaji wa kazi za  nje bila kibali cha mmiliki unaruhusiwa,hivyo alisisitiza katika uuzalisha au udurufu wa kazi yoyote iwe Muziki au Filamu ya ndani au ya nje ya nchi ni lazima kuhakikisha kuwa unamakubaliano au mikataba na mmiliki wa kazi hiyo kinyume na hapo huo ni uharamia na uvunjifu wa Sheria ya Hakimiliki.

Kwa upande wa Mtuhumiwa wa Uazilishaji ambaye ni Msimamizi wa Kampuni ya Sanyiwa Production, Frank Manyama alikiri kufanya kosa la kuzalisha kazi mbalimbali za ndani na nje ya nchi bila ya kuwa na kibali cha wamiliki wa kazi hizo.

Operesheni hiyo sehemu ya majukumu ya COSOTA katika kulinda Hakimiliki za Wasanii na kazi zote za ubunifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,409FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles