Na Anitha Jonas, Mbeya
Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) ya ahidi kuzingatia maoni ya yaliyotolewa na Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nyanda za Juu Kusini katika Kanuni mpya za Leseni ya Utangazaji na Maonesho kwa umma.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mbeya na Mwanasheria wa COSOTA, Lupakisyo Mwambinga baada ya kueleza lengo la kuundwa kwa kanuni hizo na kuwapitisha wadau hao.
“Pamoja na kwamba mtakuwa mnatoa maoni kwa kuzungumza naomba pia mjaze fomu ya maoni ili tuweze kupata maoni yenu kwa njia ya maandishi kila mmoja ajaze fomu hiyo ,tutahakikisha tunazingatia maoni yote mtakayotoa,”amesema Mwambinga.
Akizungumza katika kikao hicho cha wadau Mwambinga amesema sheria ya Hakimiliki nchini inaeleza wajibu wa watumiaji wa kazi za muziki na kulipa mirabaha hivyo suala la ulipaji wa tozo hiyo. Kwa upande wa Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mhandisi Alinanuswe John, amewapongeza wamiliki wa vyombo vya habari kwa kushiriki kikao hicho na kuwasihi wazungumze kwa hoja na waache kuwa na hasira wanapochangia hoja kwa sababu kikao hicho kimelenga kuweka mazingira rafiki ya ulipaji wa tozo hiyo ya mirabaha