26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Cosmopolitan yasaka mechi za kirafiki

GLORY MLAY-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Cosmo, Kumwembe Pazi, amesema anahitaji mechi tatu za kirafiki kwa lengo la kuendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea mzunguko wa tisa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, unaotarajiwa kuendelea Novemba 23, mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Pazi alisema wanaendelea kusaka mechi hizo kwa ajili ya kuendelea kukinoa kikosi hicho ili kiwa fikiti kwani kimekiwa kikisuasua katika mizunguko nane iliyopita.

Alisema kuwa kupitia mechi hizo kikosi chake kitazidi kuimarika kwa wachezaji kujifunza mengi ikiwamo kuzidi kuzoeana, hivyo kufanya vizuri ligi hiyo.

“Kuna timu ambazo tumepeleka maombi tunasubiri majibu kwa ajili ya kujipima, lakini  bado tunahitaji nyingine kama mbili nne hivi ili kuhakikisha tunajenga timu bora, ushindani ni mkubwa kwani kila  timu imejianda inavyoweza na sisi tunajipanga kuipande wetu kwa ajili ya ushindan huo,” alisema.

Alisema matarajio yao kuona Cosmo haishuki daraja na inabaki kwenye nafasi nzuri hata kama haitapanda Ligi Kuu msimu huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,631FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles