GLORY MLAY-DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa Cosmo, Kumwembe Pazi, amesema anahitaji mechi tatu za kirafiki kwa lengo la kuendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea mzunguko wa tisa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, unaotarajiwa kuendelea Novemba 23, mwaka huu.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Pazi alisema wanaendelea kusaka mechi hizo kwa ajili ya kuendelea kukinoa kikosi hicho ili kiwa fikiti kwani kimekiwa kikisuasua katika mizunguko nane iliyopita.
Alisema kuwa kupitia mechi hizo kikosi chake kitazidi kuimarika kwa wachezaji kujifunza mengi ikiwamo kuzidi kuzoeana, hivyo kufanya vizuri ligi hiyo.
“Kuna timu ambazo tumepeleka maombi tunasubiri majibu kwa ajili ya kujipima, lakini bado tunahitaji nyingine kama mbili nne hivi ili kuhakikisha tunajenga timu bora, ushindani ni mkubwa kwani kila timu imejianda inavyoweza na sisi tunajipanga kuipande wetu kwa ajili ya ushindan huo,” alisema.
Alisema matarajio yao kuona Cosmo haishuki daraja na inabaki kwenye nafasi nzuri hata kama haitapanda Ligi Kuu msimu huu.