24.1 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

COSATU YAMTAKA ZUMA AJIUZULU

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI


SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Afrika Kusini (Cosatu) limeunga mkono mwito wa wanaomtaka Rais Jacob Zuma ajiuzulu.

Muungano huo mkubwa kabisa wa wafanyakazi nchini humo unaojulikana kwa kukiunga mkono Chama tawala cha ANC, umemshutumu Zuma kwa visa vya ufisadi.

Miongoni mwao ni kile walichoita uhusiano wenye shaka na familia moja ya jamii ya Wahindi nchini hapa, Gupta inayodaiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika Serikali ya Zuma.

Zuma na familia hiyo ya Guptas, wamekana kufanya kosa lolote.

Wiki iliyopita chama kingine cha Kikomunisti, ambacho ni mshirika wa ANC pia kilimtaka Zuma kung'atuka madarakani kutokana na kashfa tele zinazozidi kumuandama hasa ufisadi.

Sarafu ya Rand imekuwa ukiyumba kutokana na malumbano ya kisiasa yanayoendelea hapa hasa baada ya kufutwa kazi kwa aliyekuwa Waziri wa Fedha Pravin Gordhan. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,644FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles