25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Corona yazidi kushika kasi duniani, Waingereza wawekwa karantini

BRUSSELS, UBELGIJI

MAAMBUKIZI ya virusi vya corona yanazidi kushika kasi katika maeneo yote duniani, kulingana na takwimu zinazoendelea kutolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Wakati WHO ikitoa taarifa hiyo, nchi kadhaa ikiwemo Uingereza, Afrika Kusini zimetangaza kuwakweka karantini watu wote kwa kuwaagiza kutotoka majumbani mwao, na kwa Uingereza tayari magari ya jeshi yamekuwa yakikatika katika mitaa kwa ajili ya kuwapatia wananchi mahitaji yao ya muhimu.

Kwa mujibu wa taarifa ya WHO iliyotolewa jana, maambukizi ya virusi hivyo vya Covid-19 yamefikia 332,930 kote duniani baada ya kuripotiwa maambukizi mapya 40,788 ndani ya saa 24 na vifo vimfikia 14,510 baada ya kuripotiwa vifo vipya 1727 ndani ya muda huo.

Taarifa hiyo ya WHO iliyotolewa jana iliekeza kuwa kikanda, kanda ya Magharibi mwa Pasifiki idadi ya waathiriwa ilifikia 95 637 baada ya kuripotiwa maambukizi mapya 850, ambapo idadi ya vifo ilifikia 3473 baada ya kuripotiwa vifo vipya 35 ndani ya saa 24.

Katika Kanda ya Ulaya, WHO ilieleza kuwa idadi ya wagonjwa ilifikia 171 424 baada ya kuripotiwa wagonjwa wapya 20,131 waliothibitishwa, na idadi ya vifo ilifikia 8743 baada ya kuripotia vifo vipya 1318 ndani ya saa 24.

Taarifa hiyo ya WHO jana ilieleza pia kuwa kwa Kanda ya Kusini Mashariki mwa Asia wagonjwa walifikia 1776 baada ya visa vipya 519 vya wagonjwa kuripotiwa ndani ya saa 24 na vifo kufikia 58 baada ya vifo vipya 13 kuripotiwa ndani ya muda huo.

Katika Kanda ya Mashariki mwa Mediterrania, WHO ilisema idadiya wagonjwa ilifikia 25,375 baada ya wagonjwa wapya 1706 kuripotiwa na vifo kufikia 1741 baada ya vifo vipya kuripotiwa ndani ya saa 24.

WHO ilieleza pia kuwa katika Kanda ya Amerika idadi ya wagonjwa ilifikia 37,016 baada ya wagonjwa wapya 17,331 kuripotiwa ndani ya saa 24 na vifo kufikia 465 baada ya kuripotiwa vifo vipya 213 kuripotiwa ndani ya saa 24.

Katika Kanda ya Afrika, WHO ilieleza kuwa hadi jana idadi ya wagonjwa wa corona walifikia 990 baada ya kuripotiw awagonjwa wapya 251 ndani ya saa 24 na vifo kufikia 23 baada ya kuripotiwa vifo vitatu ndani ya muda huo. 

RWANDA, UGANDA ZAFUNGA MIPAKA

Wakati WHO ikitoa taarifa hiyo, nchi mbili za Afrika Mashariki za Rwanda na Uganda zimetangaza kufunga mipaka yao yote ikiwa ni sehemu ya juhudi za kudhibiti ueneaji wa maambukizo ya virusi vya corona.

Uganda ilichukua uamuzi huo juzi baada ya nchi hiyo kuthibitisha kesi ya kwanza ya maambukizi ya virusi vya Corona, huku Rais Yoweri Museveni akiwataka wananchi wa nchi hiyo kusalia majumbani na kujiepusha kutumia usafiri wa uma.

Wakati huo huo, Rwanda imefunga mipaka yote ya nchi hiyo na watu kuamrishwa kusalia majumbani mwao katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Rwanda Jumatatu ilirekodi kesi 17 mpya za coronavirus zilizoongeza jumla ya kuwa 36, ​​Wizara ya Afya ilithibitisha.

Katika taarifa yake, Wizara hiyo ilisema kesi hizo mpya ni pamoja na wasafiri tisa kutoka UAE, watatu kutoka Kenya, wawili kutoka Marekani, mmoja kutoka Qatar, mmoja kutoka India na mawasiliano moja ya kesi nzuri iliyothibitishwa hapo awali.

“Wasafiri wote waliingia na kutengwa kati ya Machi 17-20 katika maeneo yaliyotengwa na walipimwa. Wagonjwa wote wapo chini ya matibabu katika hali nzuri, wametengwa na wagonjwa wengine. Ufuatiliaji wa mawasiliano yote umefanyika kwa usimamizi zaidi,” Wizara ilitangaza.

Hatua zingine zilizochukuliwa na Serikali ya Kigali ni pamoja na watumishi wote wa Serikali na wa mashirika binafsi kufanyia kazi nyumbani na safari za kwenda mikoani kusitishwa kwa wiki mbili kukiwa na uwezekano wa muda huo kuongezwa.

Aidha vilabu vya pombe na maduka yasiyo ya chakula pia yamefungwa huku usafiri wa bodabobda ukisitishwa.

Hatua hiyo inajiri siku moja baada ya Wizara ya Afya ya Rwanda kutangaza, watu wengine sita wameambukizwa virusi vya corona miongoni mwao mtoto mchanga wa miezi 10.

Maambukizi hayo yanaifanya Rwanda kuwa na idadi ya visa 17 vya maambukizi ya virusi vya corona.

Nchini Kenya, serikali imepiga marufuku mikusanyiko yote ya kidini, kisiasa na kijamii huku Shirika la Ndege la nchi hiyo la Kenya Airways likisitisha kwa muda safari zake zote za kimataifa kuanzia leo Jumatano ikiwa ni katika juhudi za kukabiliana na maambukizo ya virusi vya Corona.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles