24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Corona yasitisha kambi ya kitaaluma kidato cha sita Simiyu

Derick Milton, Simiyu

Siku moja baada ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kutangaza kuwepo kwa mgonjwa mmoja mwenye maambukizi ya virusi vya Corona (COVD 19) nchini, uongozi wa Mkoa wa Simiyu umesitisha kwa muda usiojulikana kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha sita.


Kambi hiyo ambayo ilikuwa ikijumuisha shule zote 10 zilizoko mkoani humo na wanafunzi 953 ambapo walianza kambi tangu Machi Mosi mwaka huu katika Shule ya Sekondari Maswa Girls iliyoko wilayani Maswa mkoani humo.


Akitangaza uamuzi huo leo Jumanne Machi 17, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Jumanne Sagini amesema mbali na kambi hiyo, kambi nyingine ndogo ambazo zinakusanya wanafunzi kutoka shule zisizozidi tatu hazitakuwepo tena.


“Kambi za shule yenyewe kwa maana wanafunzi wa shule moja, hizo zitaendelea lakini kambi ndogo na kubwa hazitakuwepo mpaka ugonjwa huu utakapoisha.


“Hata zile kambi za darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha pili, nazo hazitakuwepo lakini kama itafika Agosti ugonjwa bado upo kambi za kidato cha nne hazitafanyika maana ndiyo muda wa kambi za wanafunzi hao,” amesema Sagini.


Ameeleza hatua hiyo ya kusitisha kambi ni hatua za awali kama tahadhari ya kuepuka kuenea kwa ugonjwa huo, licha ya kufahamu kuwa kambi ni moja ya mikakati ya mkoa katika kuboresha kiwango cha elimu mkoani humo.


Kwa upande wake Ofisa Elimu Mkoa, Ernest Hinju amesema wanafunzi hao tayari waliweka kambi ya wiki mbili kati ya sita ambazo walipanga kukaa kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wao wa kitaifa 2020.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles