25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Corona yasimamisha biashara ya mbao nje ya nchi

Na Gaudence Msuya-TANGA

MENEJA wa Wakala wa Misitu (TFS) Wilaya ya Tanga, Raulence  Brighton, amesema mlipuko wa virusi vya corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu, umesababisha biashara ya usafirishaji  mbao kwenda nje ya nchi kudorora kutokana na kuzuiwa kwa safari na baadhi ya nchi kufunga mipaka yake.

Brighton alisema awali makontena ya mbao kuanzia 10 hadi  20 yalikuwa yakisafirishwa kwa kila mwezi kupitia bandari, lakini sasa biashara imesimama.

Alisema usafirishaji wa mbao umetibuka baada ya kutangazwa kwa mlipuko wa corona katika nchi za Ulaya na Marekani ambako ndipo kwenye soko kubwa la bidhaa hiyo.

 “Hali siyo nzuri kwa biashara ya mbao, corona imesababisha kufungwa kwa safari na mipaka na hivyo kushindwa kuendelea kufanyika, na hii itategemea maendeleo ya udhibiti wa ugonjwa huo,” alisema Brighton.

Alisema kwa kipindi cha mwaka 2018/19  TFS jijini Tanga ilikamata magogo yaliyokuwa yakisafirishwa visivyo halali yenye thamani ya Sh milioni 240  ambayo alidai watuhumiwa walifikishwa mahakamani na kushindwa kesi.

Brighton alisema baada ya uamuzi wa mahakama, TFS ilitowa tangazo la mnada ambao alisema uliharibika baada ya aliyeshinda kushindwa kulipa gharama za magogo hayo.

Meneja wa TFS  Wilaya ya Mkinga, Arcado Ngumbala alieleza mkakati wa kuanzisha shamba jipya eneo la Mwakijembe wilayani humo lenye ukubwa wa hekta 8,979 na kwa mwaka huu hekta kumi zimeshaanza kuendelezwa.

Naye  Meneja wa TFS  Kanda ya Kaskazini, Edward  Shilogile, alisema walivuka lengo kwa kukusanya Sh bilioni 6.6 kwa mazao ya kwa mwaka 2019/20.

Shilogile pia alitumia nafasi hiyo kuwatahadharisha  watumishi wasio waaminifu wanaosaidia kuhujumu mali za misitu ikiwemo kuuza mbegu ambazo zinatolewa bure kwa watu waliotimiza vigezo vinavyotakiwa.

Alieleza kuwa kufanya hivyo ni kosa kwa sababu Serikali imegharamia mbegu hizo na hivyo kinachotakiwa ni watumishi hao kutoa elimu kwa wananchi wanaohitaji ili kukidhi vigezo vya kupatiwa miche hiyo bila kununua.

Alikemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wasio waaminifu kutega mitego kwenye hifadhi ya Rau iliyopo Moshi kwa lengo la kunasa wanyama jambo ambalo alilieleza kuwa ni kosa na kwamba atakayepatikana atachukuliwa hatua za kisheria.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,540FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles