25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Corona yapunguza magonjwa ya mlipuko

Na Raymond Minja

Magonjwa ya mlipuko katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ikiwemo kipindupindu, kuhara pamoja na mafua yamepungua kwa kiasi kikubwa baada ya janga la corona kupita kutoka na jamii kuelimika kuhusu unawaji mikono kwa sabuni na maji tiririka.

Akizungumza na leo Novemba 6, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mafinga Mji, Dk. Victor Msafiri amesema hospitali hiyo kwasasa imekuwa ikipokea wagonjwa wachache sana wa magonjwa ya mlipuko kutokana na wananchi kujitambua kwa kuchukua tahadhari.

Msafiri amesema kabla ya ugonjwa huo kuingia nchini, hospitali hiyo ilikuwa ikipokea wangonjwa wengi wa magonjwa ya mlipuko kama kuharisha, homa ya matumbo, mafua pamoja na nimonia kutokana na watu wengi kutokuchukua tahadhari.

“Suala la unawaji mikono kwa kutumia maji tiririka na kuvaa barakoa kwa kweli magonjwa mengi yamepungua mfao, mafua yamepungua maana watu wanavaa barakoa, magonjwa ya kuhara yamepungua maana watu siku hizi wananawa mikono kwa hiyo corona imefanya Watanzania kuwa na utamaduni wa kunawa mikono jambo lililosaidia magonjwa mengi kupungua kwa kiasi kikubwa,”amesema Dk. Msafiri.

Amesema kutokana na mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Taasisi nyingi zikiwemo hospitali na Shule waliweka vifaa vya kunawia mikono pamoja na sabuni jambo lililosaidia kupunguza magonjwa ya milipuko kwa kiasi kikubwa.

Aidha, Msafiri aliwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo hata kama unaonekana kuisha

“Niwaombe tuendelee kunawa mikono kwa maji na sabuni kwani wenzetu wa Kenya, Uganda na Burundi bado huu ugonjwa upo na ikumbukwe kuwa watu wengi wanakuja kufanya biashara zao hapa nchini hivyo tahadhari ni jambo muhimu kwani unaweza kurudi wakati wowote,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,454FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles