26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Corona yapunguza kiwango cha uchangiaji damu

AVELINE  KITOMARY, DAR ES SALAAM

Mpango wa Taifa wa Damu Salama  umesema kuwa kutokana na janga ya mlipuko wa virusi vya corona(Covid-19) nchini  kiwango cha uchangiaji damu kimeshuka  kutoka chupa 31,502 za mwezi Februari, chupa 25,737 za mwezi Machi  hadi kufikia chupa 22,044 Mwezi Aprili.

Akizungumza wakati wa Semina ya Waandishi wa habari za Afya kuelekea maadhimisho ya siku ya Wachangiaji damu Duniani Juni 14,Meneja wa mpago wa damu salama kanda ya mashariki ,Dk Avelina Mgasa,amesema hali hiyo imechangiwa  na shule na vyuo  kufungwa  hivyo kukosa fursa za  kukusanya damu  katika ofisi mbalimbali.

“Kingine ambacho kimesababisha ukasanyaji wa damu kuwa mdogo ni zuio la mikusanyiko kutokana na maelekezo ya serikali katika kupambana na Covid-19 kwani maeneo hayo ndiyo yamekuwa yakitegemewa zaidi,”amesema.

Dk Mgasa amesema hivi sasa wamejipanga  katika kuhakikisha watu wanachangia damu katika mazingira salama ambayo yatawawezesha kujikinga na Covid-19.

“Kutokana na hilo basi uhitaji wa damu ni mkubwa sisi kama damu salama tumejipanga  kwani uchangia wa damu ni tendo salama na mpango umeweka mikakati mbalimbali ya kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona katika vituo vya kuchangia damu.

“Tumuweka maji tiririka na sabuni kwaajili ya kunawa mikono,Vitakasa mikono,Vifaa kinga kwa watumishi kama barakoa, apron/koti, gloves, na goggles,Thermo scanner kwaajili ya kupima jotoridi la mwili kwa kila mchangia damu.

“Tunatakasa vitanda na vifaa vinavyotumika na wachangia damu,mpangilio unaozingatia umbali kati ya mtu na mtu (social distance),”ameeleza Dk Mgasa.

Amesema kwa mwaka huu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsi,Wazee na Watoto ,Ummy Mwalimu, ataongea na wananchi na kuwashukuru wachangia damu.

Kaulimbili katika maadhimisho hayo ni Damu Salama Inaokoa Maisha, “Safe Blood Saves Lives”.

Amesema malengo ya kampeni wakati wa maadhimisho

Hayo ni kukusanya chupa za damu 24,800 .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles