26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Corona yaongeza matumizi ya TEHAMA mahakamani

Na Amina Omari, Tanga

Mlipuko wa ugonjwa wa corona nchini umeongeza kasi ya matumizi ya teknolojia katika ngazi ya mahakama na kurahisisha utoaji wa maamuzi katika mashauri mbalimbali ya kesi.

Hayo yamebainishwa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Amir Mruma wakati akigawa vitendea kazi ikiwamo kompyuta mpakato (laptop) kwa Mahakimu 53 wa mkoa huo kwa ajili ya kuwasaidia kuendesha na kusikiliza kesi kwa njia ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Amesema ugonjwa huo ulioshika kasi hapa nchini mwanzoni mwa mwaka huu, umebadilisha kwa kiasi kikubwa hata namna ya kuendesha kesi kwani wafungwa hawakulazimika kusafiri umbali mrefu kuja mahakani ili kusikiliza mashauri yao.

“Corona imesaidia hata kupunguza changamoto mahabusu kutofika kwa wakati kutokana na changamoto ya ukosefu wa usafiri na hivyo tulilazimika kutumia mfumo wa TEHAMA kusikiliza mashauri yote,” amesema Jaji Mruma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles