28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Corona yaondoa maisha ya Allen Garfield

LOS ANGELES, MAREKANI

STAA wa filamu nchini Marekani, Allen Garfield, amefariki dunia kutokana na virusi vya Corona, huku akiwa na umri wa miaka 80.

Mkali huyo alitamba katika filamu mbalimbali ikiwa pamoja na Beverly Hills Cop II ambapo ndani yake alikuwa staa mwingine Eddie Murphy.

Dada wa msanii huyo Lois Goorwitz, amethibitisha kifo hicho kwa kuweka wazi kuwa virusi vya Corona ndio chanzo cha kifo chake.

“Mpendwa wetu, ndugu yetu, baba yetu amepoteza maisha, alikuwa mwalimu wa wengi kutokana na kile ambacho alikuwa anakifanya kwenye filamu, hata wakati anaingia kwenye tasnia hiyo lengo lake kubwa lilikuwa ni kuja kuwa mwalimu wa filamu, hivyo wengi wamejifunza kutoka kwake, lakini kwa sasa hayupo tena nasi,” alisema dada wa msanii huyo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles