27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Corona yamvaa kocha Uturuki, yamuibua Mourinho

ANKARA, Uturuki

KOCHA wa Galatasaray inayoshiriki Ligi Kuu ya Uturuki, Fatih Terim, amefichua kuwa ni mwathirika wa virusi vya Corona vinavyoendelea kuutikisa ulimwengu.

Wakati huo huo, mkuu wa benchi la ufundi la Tottenham, Jose Mourinho, amejitokeza kuwasaidia wazee waliopata maambukizi ya virusi hivyo jijini London, Uingereza.

Mourinho

Mourinho alionekana akiwa akipakia vyakula kwenye mifuko, ambavyo vilikwenda katika maeneo waliyoko wazee, mpango unaoendeshwa na taasisi za Age UK na Love Your DoorStep.

Kwa upande wa Terim aliyewahi kuinoa AS Milan na timu ya taifa ya Uturuki, alitumia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa twitter kuthibitisha kuwa ameambukizwa virusi hivyo.

“Majibu ya vipimo vya virusi vya Corona vimeonesha kuwa ni mwathirika,” aliandika Terim, ambaye hivi karibuni bosi wake, ambaye ni Makamu mwenyekiti wa klabu ya Galatasaray, Abdürrahim Albayrak, naye aliripotiwa kupata maambukizi.

Kabla ya kusimamishwa mwishoni mwa wiki iliyopita, Ligi Kuu ya Uturuki ilikuwa ikiendelea kuchezwa bila mashabiki na Terim alikuwa mmoja kati ya waliokuwa wakilaani kitendo hicho.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles