25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Corona itaacha ukata VPL, FDL

Zainab Iddy, Dar es Salaam

BAADA ya Serikali kusimamisha  Ligi Kuu Tanzania Bara sambamba na michezo mingine yote kwa siku 30 , baadhi ya wachambuzi wa soka nchini wamesema kuwa   suala la ukata halitokwepeka  pale mashindano yatakapoendelea.

Juzi Serikali kupitia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , alitangaza kusitisha shughuli zote zinazosababisha mikusanyiko ya watu ikiwemo michezo kama njia ya kuchukua tahadhari ya kuenea kwa ugonjwa wa Corona ulioonekana kuwa janga  ulimwenguni kote.

Wakizungumza na MTANZANIA jana, kwa nyakati tofauli wachambuzi hao walisema  ni jambo zuri lililofanywa na serikali lakini lazima Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lifahamu pale ligi zitakapoendelea kutakuwa na tatizo kubwa la uchumi kwa wanachama wao.

“Kila mmoja nafahamu jinsi  baadhi ya timu zilivyokuwa zinaendeshwa kiugumu hadi baadhi kushindwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine, hivyo kusimama kw aligi kutaongeza maumivu zaidi ya yale ya kwanza.

“Bila shaka kuna  timu zilishapambana kutafuta fedha zitakazoweza kuwasaidia kumaliza ligi, walipozipata walilipa gharama mbalimbali hadi mwisho wa msimu  kabla ya muda kufika yametokea haya ni vigumu kurejeshewa gharama zao kama walivyotoa,

“Lakini pia wamelazimika kuwapa nauli wachezaji ili warejee  katika familia zao, hivyo watata kiwa kuja kuwarejesha pia, hii ni kazi mara mbili,” alisema Ally Mayay.

Kwa upande wake, Alex Kashasha alisema : “ Bajeti iliyokuwa imedundulizwa haikuwa inatosha, kwa hili lililotokea timu lazima ziingie gharama kwa sababu siku zote inapotoka ratiba huwa zinajipanga kulingana na ratiba,  kutokana na mabadiliko haya TFF ijiandae kupokea kesi nyingi za madai.

“ Madhara mengine yataonekana kwa wachezaji mmoja mmoja, bila shaka viwango vyao vitashuka kwa sababu muda mwingi watakuwa katika nyumba zao na wachache watakuwa na akili ya kufanya mazoezi binafsi hili litasababisha ligi ijayo au itakapoendelea kupoteza mvuto,”alisema Kashasha.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles