MWIGIZAJI wa filamu za Bongo, Baby Joseph Madaha, yupo mbioni kuachia wimbo wake mpya wa ‘Corazon’.
Baby Madaha alisema kwa sasa anamalizia video ya wimbo huo ambao picha zake zinapigwa huko Dubai na unatarajiwa kukamilika mwezi ujao.
“Nipo kwenye harakati za mwisho za kukamilisha video ya wimbo wangu mpya wa ‘Corazon’ unaomaanisha moyo wangu ambao nimeufanyia Dubai na ninaomba mashabiki wangu waendelee kuniombea ukamilike kama nilivyopanga,” alisema.
Madaha aliongeza kwamba, wimbo huo ameurekodia katika studio za prodyuza mkali katika midundo nchini, Christopher Kanjenje (C9).