24.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 29, 2023

Contact us: [email protected]

CONTE HATAKUWA NA MUDA MREFU WA KUFUNDISHA

LONDON, ENGLAND


 

antonio-conteKOCHA wa vinara wa Ligi Kuu nchini England, Chelsea, Antonio Conte, ameweka wazi kuwa anapenda kufundisha soka, lakini hana uhakika wa kuendelea kufanya hivyo kama ilivyo kwa kocha wa zamani wa Man United, Sir Alex Ferguson na kocha wa sasa wa Arsenal, Arsene Wenger.

Conte amesema alikuwa anavutiwa sana na uwezo wa Ferguson ambaye aliifundisha United kwa miaka 27 tangu 1986 hadi 2013 alipotangaza kustaafu, hivyo kocha huyo alidumu kwenye klabu hiyo kwa muda mrefu.

Hata hivyo, Conte amedai kuwa kocha mwingine ambaye amedumu kwenye klabu moja kwa muda mrefu ni pamoja na Arsene Wenger, ambapo hadi sasa amefikisha miaka 20 ndani ya klabu hiyo.

Conte amesisitiza kuwa anatamani kufikia hatua ambayo Ferguson alifikia ndani ya United, lakini kwa upande wake amedai anatarajia kustaafu huku akiwa na umri mdogo sana si kama ilivyo kwa Ferguson na Wenger.

Wakati huo Mkurugenzi wa klabu ya Chelsea, Michael Emenalo, amedai kuwa kocha huyo ataendelea kuwa Stamford Bridge hadi mwisho wake wa kufundisha soka kama alivyofanya Ferguson.

Ferguson katika kipindi chake alifanikiwa kutwaa mataji 13 ya Ligi Kuu nchini England, pamoja na mataji mawili ya Klabu Bingwa Ulaya. Conte amesisitiza kuwa na ndoto za mafanikio kama kocha huyo pamoja na Wenger.

“Hapa nazungumzia miamba miwili ya soka duniani katika ufundishaji, kwa upande wangu makocha ambao wananifanya niwafikirie ni Sir Alex Ferguson, ni mfano kwangu.

“Kila nikimwangalia yeye na Wenger natamani nifikie mafanikio yao, ninaamini siwezi kufikia walipofikia wao, lakini kwa upande wangu miaka 10 inatosha kabisa katika soka, lakini miaka 20 mbele itakuwa ngumu kwa kuwa hapa nilipo nina miaka 47, najua soka ni maisha yangu lakini sitafika huko.

“Kutokana na hali hiyo nitahakikisha ninafanya makubwa kwa kipindi ambacho kitakuwepo katika soka ili kuweza kuzisaidia klabu ambazo nitakuwa nazifundisha kwa kipindi hicho chote,” alisema Conte.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles