LONDON, ENGLAND
KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte, ameonesha imani yake kuhusu kiwango cha winga wake, Eden Hazard, kuongezeka licha ya kuanza vibaya mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.
Hazard alikosa michezo ya mwanzo wa msimu baada ya kufanyiwa upasuaji katika kifundo cha mguu lakini amerejea uwanjani baada ya kupona.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 26, alikuwa msaada mkubwa katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Newcastle United, akishinda mabao mawili.
Lakini Conte anaamini kuna mambo mazuri makubwa yanakuja kutoka kwa wachezaji wake huku akimtaja Hazard kutumia tuzo ya mchezaji bora ‘Ballon d’Or’ na michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kama njia ya kuboresha kiwango chake.
“Sifikirii kama Hazard amefika kwenye kiwango chake cha ubora, ana mambo mengi ya kuyatarajia, bado ni mchezaji mdogo na muhimu kufanya kazi, kujituma katika kila mazoezi ili kuboresha kiwango chake ili kurejea kama zamani. Unakuwa bora zaidi ukishinda tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya kwanza, ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya pamoja na Kombe la Dunia.
“Michuano ya Kombe la Dunia ni mikubwa sana, katika michuano hiyo unaweza kuonesha uwezo wako, ” alisema Conte.
Lakini Conte alimuonya Hazard kuhusu mbinu yake ya upigaji wa penalti, wakati nyota huyo alipopata nafasi ya kupiga penalti dhidi ya Newcastle.
“Wakati nachukua mpira katika mikono yangu ni jambo jingine, nataka kufanya hivyo, nahitaji kipa apotee eneo lake kama hatafanya hivyo nitakuwa kwenye matatizo,” alisema Hazard.