28.3 C
Dar es Salaam
Saturday, November 26, 2022

Contact us: [email protected]

Conte akiri timu yake dhaifu

 kocha wa  timu ya Chelsea, Antonio Conte
kocha wa timu ya Chelsea, Antonio Conte

LONDON, ENGLAND

BAADA  ya  kupata pointi moja  katika michezo mitatu  ya Ligi Kuu England, kocha wa  timu ya Chelsea, Antonio Conte, jana aliwapa  onyo  wachezaji wake kwa  kuwataka warejee katika  viwango vyao.

Kocha huyo aliwajia juu wachezaji wake hao baada ya kushuhudia  juzi wakifungwa jumla  ya mabao 3-0 wakiwa uwanja wa ugenini.

“Chelsea  ni timu kubwa katika makaratasi tu, lakini si  uwanjani, nataka iwe kubwa hata  uwanjani kwani uwanja ndio sehemu sahihi kwa kuwa huko ndio sehemu inayofaa kuonesha uwezo.

“Kujituma na kupata matokeo mazuri ndio kitu muhimu ambacho ninichokitaka, hivyo tunatakiwa kufanya kazi ya ziada ili tufikie malengo,” alisema Conte.

Conte alisema msimu uliopita ulikuwa mbaya kwao na kuongeza kuwa hawatakiwi kufanya makosa waliofanya katika msimu huo, badala yake wanatakiwa kutafuta suluhisho sahihi ili kupata mwelekeo mzuri wa kupata ushindi msimu huu.

“Tunajua kuna vikwazo vingi katika  kufikia lengo na hatujapata uwiano mzuri, ni muda sasa wa kusahihisha kila kitu kwani haikuwa sahihi kwetu kuruhusu kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Arsenal,” alisema Conte.

Mchezo dhidi ya Liverpool, Chelsea haikuwa katika kiwango kizuri kwani ilianza kuruhusu bao dakika ya 36 pia  hali hiyo ilijitokeza hata katika mchezo wa Kombe la Ligi ya England (EFL), dhidi ya Leicester City walipoanza kufungwa dakika ya 34 kabla ya kupambana kupata ushindi dakika ya nyongeza.

Chelsea wamepata mabao 13 katika michezo nane ikiwa michezo saba bila ya beki wa timu hiyo, John Terry mwenye umri wa miaka 35.

Katika mchezo dhidi ya Arsenal, Conte alisita kumtupia lawama beki wake, Gary Cahill na kudai kuwa  kila mmoja anatakiwa  kuhusika na kipigo hicho.

Beki huyo  anadaiwa  kushindwa kufuata maelekezo ya kocha huyo hasa  kipindi cha pili,  ambapo alimtaka kucheza  beki namba tatu.

“Tunatakiwa  kutafuta  suluhisho, kupoteza katika michezo miwili mikubwa, Liverpool na Arsenal.

“Kwa sababu hiyo, tunatakiwa  kuelewa  hali tuliyonayo, tunatakiwa kufanya kazi ili kuboresha kiwango chetu na kubadili historia,” alisema Conte.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,558FollowersFollow
557,000SubscribersSubscribe

Latest Articles