26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Congress yamtia hatiani Trump

WASHINGTON, MAREKANI

BUNGE la Marekani (Congress) limepasisha kwa wingi wa kura muswada wa kumwita Raos Donald Trump wa nchi hiyo bungeni kujieleza, baada ya kumpata na hatia katika kashfa ya “Ukraine Gate”.

Wabunge hao wa Marekani wamepasisha kwa kura nyingi muswada huo wa kumwita rais huyo wa 45 wa Marekani bungeni hapo, akiwa ni rais wa tatu wa Marekani katika historia ya nchi hiyo kuitwa bungeni kujieleza.

Rais Trump anakuwa rais wa tatu wa Marekani kutiwa hatiani na baraza hilo, baada ya Rais Andrew Johnson mwaak 1869, na Bill Clinton ambapo mmoja, Richard Nixon aliwahi kujiuzulu kabla ya kupigiwa kura mwaka 1974.

Katika kura hiyo iliyopigwa usiku wa kuamkia jana, wabunge hao walipasisha muswada huo kwa kura 230 za ndio kwa 197 za hapana kwa kosa la Trump kutumia vibaya madaraka yake, na kura 229 za ndio kwa 198 za hapana kwa kosa la kuzuia uchunguzi wa bunge la Congress.

Awali, Kamati ya Mahakama ya Bunge la Marekani ilikuwa imeunga mkono na kupasisha tuhuma kwamba Trump ametumia vibaya madaraka yake na pia amefanya njama za kulizuia Bunge kufanya uchunguzi kuhusu kashfa zinazomkabili.

Miswada hiyo itapelekwa kwa Baraza la Sanate la Marekani kupigiwa kura kabla ya kuanza kikao cha kumuhukumu Trump.

Baraza la Sanate la Marekani litachunguza miswada hiyo mwezi Januari mwakani, yaani 2020.

Mchakato wa kumwita bungeni Trump ulianza baada ya kufichuliwa kashfa ya mazungumzo ya simu kati yake na Rais wa Ukraine, ambapo katika mazungumzo hayo, Trump alimtaka rais huyo wa Ukraine afanye uchunguzi wa siri wa kufichua kashfa za mpinzani wa Trump, Joe Biden katika uchaguzi ujao wa Rais wa Marekani, kama Ukraine inataka kupata misaada ya Marekani.

Chama cha Democrats kinaamini kwamba Trump hadi hivi sasa amefanya mambo mengi yaliyo kinyume na Katiba ya nchi hiyo.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya Baraza la Wawakilishi la Marekani kumshitaki Rais Donald Trump, Spika wa Baraza hilo aliyesimamia muswada huo, Nancy Pelosi alikataa kusema kwa uhakika, muda ambao atawasilisha vifungu viwili vya mashtaka ndani ya baraza la Seneti kwa ajili ya hukumu.

Maoni yake yalikuja kama mshangao wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliokusudia kutoa ujumbe wa Democratic baada ya kupiga kura ya kumshitaki Trump kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Pelosi aliwasifu Wademocratic wenzake akisema ilikuwa ni siku kubwa kwa ajili ya katiba ya Marekani.

Muda mfupi baada ya uamuzi huo, Spika Pelosi alituma ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter akimuambia Trump kwamba hakuna aliye juu ya sheria.

Mwakilishi wa Michigan kwenye Baraza hilo la Wawakilishi, Daniel Kildee, aliita jana kuwa siku ya huzuni lakini muhimu.

“Ninasikitika kwa sababu nyingi lakini pia nimeridhika kujuwa kwamba kwenye nchi hii unaweza kumuwajibisha mtu yeyote aliyechaguliwa kupitia katiba. Hakuna anayefurahia hili, lakini inapendeza kuona kwamba Katiba yetu inafanya kazi,” alisema Kildee.

Kesi hiyo dhidi ya Rais Trump inatarajiwa kuanza mwezi Januari katika Seneti, ambako theluthi mbili inahitajika kwa ajili ya kumuondoa madarakani.

Bunge la Seneti linadhibitiwa na chama cha Republican cha Rais Trump.

Trump aendeleza ubabe

Muda mfupi baada ya Baraza la Wawakilishi kupitisha uamuzi huo wa kumshitaki,  Rais Trump mwenyewe aliitisha mkutano wa hadhara kuwashambulia vikali wajumbe wa Democrat waliopiga kura hiyo.

Trump alihutubia mkutano wa hadhara katika jimbo la Michigan, ambako kwenye hotuba yake ya masaa mawili alitumia muda mrefu kuwashutumu wajumbe wa Democrat, akiwemo Spika Pelosi, kwa kile alichokiita “maandamano ya kujitoa muhanga.”

Alisema kura ya kumshitaki ilikuwa ni aibu kwa Taifa la Marekani.

rump alikuwa akihutubia mkutano wa wafuasi wake.

Image caption

Trump aliwaambia watu wa Michigan kuwa “Wakati tunabuni ajira na kupambana kwa ajili ya Michigan, wenye itikadi kali za mrengo wa kushoto katika Kongresi wamejawa na wivu na chuki na hasira kubwa, unaona kile kinachoendelea.”

Aliuambia umati wa watu waliokua wamekusanyika katika eneo la Battle Creek, jimboni Michigan kwamba: “Wakati tunabuni ajira na kupambana kwa ajili ya Michigan, wenye itikadi kali za mrengo wa kushoto katika Congress wamejawa na wivu na chuki na hasira kubwa, unaona kile kinachoendelea.”

Ikulu ya White House ilitoa taarifa inayosema kuwa rais “ana imani kwamba atasafishwa na tuhuma zote” katika kesi hiyo kwenye Bunge la Seneti.

Seneta wa New York kutokea Republican, Peter King, alisema kwamba Democrat wametumia kura yao kama silaha na sio kwa sababu Trump ana makosa anayoshukiwa nayo.

“Ni bahati mbaya na ni kuweka kigezo cha hatari. Tunatumia kesi dhidi ya rais kama silaha. Kufanya hivi ni hatari sana. Nilipiga kura dhidi ya kumshitaki Clinton. Nitapiga kura dhidi ya kumshitaki Trump,” alisema King.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles