23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Congo waitabiria makubwa Kenya

MADRID, HISPANIA

KOCHA wa timu ya taifa ya DR Congo, Florent Ibenge, anaamini timu ya Kenya, Harambee Stars ina nafasi kubwa ya kufika mbali kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika nchini Misri kutokana na ubora wa kikosi chao.

Juzi timu hizo zilicheza mchezo wa kirafiki wa kupima nguvu vikosi vyao kuelekea michuano hiyo na kutoshana nguvu kwa kutoka sare ya bao 1-1 huko nchini Hispania.

Kocha huyo ameweka wazi kuwa, alivutiwa na kiwango cha wapinzani wao, hivyo anawapa nafasi kubwa ya kufanya vizuri.

“Kenya wana timu bora kutokana na kuwa na wachezaji wengi wazuri, hivyo mchezo wetu wa kirafiki ulikuwa ni kipimo sahihi na ninawatakia kila la heri kwenye michuano hii ya Afcon.

“Katika kipindi cha kwanza walikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu, hivyo ninaamini kwenye michuano hiyo ya Afcon wataacha alama endapo watacheza kama walivyocheza na sisi,” alisema Ibenge.

Kwa upande wa timu ya DR Congo, kocha huyo ameweka wazi kuwa, lazima afanye mabadiliko ya kikosi chake kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ili kuleta ushindani mkubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles