24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

Coca-Cola yazindua kinywaji kipya cha Schweppes+C


Na MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Coca-Cola Tanzania, imezindua kinywaji kipya chenye ladha ya limao kinachojulikana kama Schweppes +C, ikiwa ni sehemu ya kuongeza chaguo la bidhaa kwa wateja wake.

Kinywaji cha Schweppes+C kinawalenga zaidi wateja wenye umri mkubwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kinywaji hicho Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa  Coca-Cola, Basil Gadzios, alisema kampuni yake imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye ugunduzi na kuongeza idadi ya bidhaa tofauti tofauti ikiwa na lengo la kukidhi mahitaji ya wateja katika soko la Tanzania.

“Tunayo furaha kuongeza bidhaa nyingine mpya sokoni, ikiwa ni shehemu ya jitihada za kukidhi mahitaji ya wateja wetu. Schweppes+C yenye ladha ya limao inawaletea wateja wetu ladha ya kipekee ya limao ikiwa na Vitamini C ambayo tunaamini wataifurahia.

Kinywaji hiki kimetengenezwa mahsusi kumpa mtumiaji wake ladha nzuri ya juisi ya limao. Tukiwa kama kampuni ya vinywaji baridi, tumejizatiti kuwaletea wateja wetu kilicho bora na bado tuna vingi kwa ajili yao,” alisema mkurugenzi huyo.

Aidha, Gadzios aliongeza kuwa, Kampuni ya Coca-Cola inatarajia kuingiza sokoni bidhaa nyingine nyingi ambazo si tu zitakidhi mahitaji ya jamii ya leo, bali pia zitaendana na mahitaji ya wateja ambayo hubadilika huku akiongeza kuwa kinywaji hicho kipya kimetengenezwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa kikiwa na ladha ya kipekee ya limao.

“Kuwashirikisha wateja wetu ni moja kati ya vipaumbele vya Kampuni ya Coca-Cola. Hii inatusaidia kuyafahamu mahitaji yao ambayo hubadilika kulingana na muda na  hivyo kutuwezesha kuwaletea bidhaa zinazoendana na mahitaji na matakwa yao.

“Kuongezwa kwa Vitamin C kwenye kinywaji kipya cha Schweppes +C, kunakifanya kinywaji hiki kitofautiane na vinywaji vyetu vingine vilivyopo sokoni huku kikiwapa wateja ladha murua ya limao,” alieleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles