Coastal Union watoa siri ya kutoa vichapo

0
843
Kiungo wa Yanga, Mapinduzi Balama(kushoto), akimtoka Ayub Lyanga wa Coastal Union, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda bao 1-0, lililofungwa na kiungo, Abdulaziz Makame. Picha na Loveness Benard.

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

MCHEZAJI wa Coastal Union, Shaban Idd, amesema kwa mfumo wanaoutumia kwa sasa, timu yoyote watakayokutana nayo, haitatoka salama zaidi ya kupata kichapo.

Coastal Union juzi waliendeleza ushindi baada ya kuinyuka Kagera Sugar bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Ushindi huo ni wa sita mfululizo kwa timu hiyo, wakianza kwa kuichapam Ndanda FC bao 1-0, Namungo FC (3-1) kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi, Azam FC (1-0), Mbeya City (2-0) na Tanzania Prisons (1-0).

Akizungumza juzi baada ya mchezo huo wa juzi, Idd alisema kwa sasa timu yao imebadilika kwani wamekuwa wakipata matokeo tofauti na nyuma hali inayowaongezea morali ya kuzidi kupambana.

“Tunashukuru timu yetu inapata matokeo mazuri kwa sasa kutokana na kubadilisha mfumo wa kucheza ambao unafanya kila timu tunayokutana nayo, haitoki salama mbele yetu,” alisema.

Alisema wataendelea kucheza kwa umoja ili wafanye vizuri na kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here