Ciara afurahia kusubiri mtoto wa tatu

0
735
52342529 Superstar couple Russell Wilson and Ciara were seen doing some shopping together and stopping to grab a bite to eat in West Hollywood, California on March 11, 2017. Ciara showed off her growing baby bump and Russell showed off his sweet ride as the two of them pulled up in a classic Rolls-Royce convertible. FameFlynet, Inc - Beverly Hills, CA, USA - +1 (310) 505-9876

New York, Marekani

STAA wa muziki nchini Marekani, Ciara Harris, ameweka wazi kuwa na furaha ya kuongeza familia yake huku akiwa anasubiri mtoto wa tatu miezi ya hivi karibuni.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 34, alifanikiwa kufunga ndoa na nyota wa soka nchini Marekani, Russell Wilson tangu mwaka 2016.

Wawili hao walifanikiwa kupata mtoto wa kwanza miaka miwili iliopita na sasa wanatarajia mtoto wa pili, lakini Ciara alipata mtoto wa kwanza akiwa kwenye uhusiano na rapa Future.

“Nimekuwa nikipenda sana watoto, furaha yangu ni kuona ninakuwa na familia kubwa, nasubiri kwa hamu mtoto wangu wa tatu,” aliandika mrembo huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akiposti picha mbalimbali za kuonesha tumbo lake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here