25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Chuo kufundisha masuala ya uchawi

VARASANASI, India

CHUO maarufu nchini India, kimeanza kutoa kozi ya ngazi ya cheti kwa madaktari jinsi ya kutibu wagonjwa wanaopatwa mapepo au huyaona.

Kozi hiyo ya miezi sita katika chuo kikuu cha Banaras Hindu (BHU), kwa mji wa kaskazini wa Varasanasi, itaanza mwezi huu.

Pia kozi hiyo, itakuwa inatolewa na kitengo cha afya ya akili na magonjwa yasiyo ya kawaida.

Msemaji wa chuo, aliambia shirika la habari la India kuwa kitengo cha masomo ya uchawi kimeanzishwa.

”Kitengo hicho kinaitwa Bhoot Vidya,kunajihusisha na magonjwa yasiyo ya kawaida ama matatizo ya akili” anasema Yamini Bhushan Tripathi mkuu wa kitengo hicho.

Aliongeza pia chuo hiki ndiyo chuo cha kwanza kuanzisha kozi ya namna hiyo ambayo itafundisha masomo ya utabibu wa majini, mapepo na mizimu.

Matibabu yatatolewa kwa njia ya dawa za asili, miti shamba na masaji.

Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2016 wa kitengo cha magonjwa ya akili (Nimhans) karibu asilimia 14 ya watu nchini humo, ni wagonjwa wa akili na mwaka 2017 Shirika la Afya Duniani (WHO), inakadiria asilimia 20 ya Wahindi wanaweza kupatwa na msongo wa mawazo katika kipindi fulani katika maisha yao.

Lakini kuna chini ya wagonjwa 4,000 wa akili huwa wanaenda hospitali kupatiwa matibabu rasmi, kuna uelewa mdogo sana juu ya afya ya akili.

Kutokana na unyanyapaa kusambaa,wagonjwa wachache ndiyo wanaenda hospitali wengi huenda kwa waganga wa kienyeji na kudhani kuwa watatibiwa matatizo yao ya akili.

Wengi wameonesha kulidhihaki tangazo hilo katika mitandao ya kijami, baadhi wameuliza Serikali ya India je vipaumbele vyake vikwapi?

Taarifa ya chuo hicho cha serikali kitaanza kutoa kozi hiyo, imepokelewa kwa maoni mbalimbali katika mitandao ya kijamii, wengi wakiuliza ni namna gani kozi hiyo itatolewa?

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles