31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Chuo Kikuu Mzumbe chawakaribisha Wanafunzi na Wawekezaji Mnazi Mmoja

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Chuo Kikuu cha Mzumbe kimewakaribisha wanafunzi wa wanaotaka kusoma fani mbalimbali mbalimbali kutembelea banda lake ili kujua programu mbalimbali zinatolewa na chuo hicho ikiwamo ushauri wa kitaalamu.

Dk. Faida Fundi wa Shule ya Utawala na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe(kulia) akitoa maelekezo kwa mmoja wa wanafunzi aliotembelea banda la chuo hicho katika maonyesho ya Vyuo vya Elimu ya Juu yanayoendela katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Aidha, chuo hicho pia kimewakaribisha wawekezaji wanaotka kuwekeza kwenye chuo hicho kutembelea banda hilo kwa ajili ya kufahamu sera yake ya uwekezaji.

Hayo yamebainishwa Julai 18, 2022 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa chuo hicho, Rose Joseph wakati akizungumza na Mtanzania Digital katika maonyesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam yakihusisha vyuo mbalimbali.

Rosema amesema chuo hicho kina zaidi ya programu 44 kuanzia ngazi ya Stashahada hadi Shahada ya Uzamivu(PhD) ambapo mwanafunzi akifika kwenye banda lao atapatiwa msaada wa kitaalamu juu ya fani anayotaka kusoma.

Dk. Issaya Lupogo ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe (kushoto) akitoa maelekezo kwa mmoja wa wanafunzi aliotembelea banda la chuo hicho(kulia) katika maonyesho ya Vyuo vya Elimu ya Juu yanayoendela katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

“Chuo Kikuu Mzumbe tunashikiriki katika haya maonyesho ya Vyuo Vikuu ambayo yameandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU), na kikubwa tunachokifanya hapa ni kuweza kuwafamisha wanafunzi na Watanzania kwa ujumla juu ya programu zetu zaidi ya 44 ambazo tunatoa kuanzia ngazi ya Stashahada hadi Shahada ya Uzamivu.

“Hivyo mwananchi ambayo anataka kujua zaidi juu ya programu hizi tunazozitoa tunamkaribisha Mnazi Mmoja ndani ya banda letu kwa ajili ya kupata mwongozo kutoka kwa wataalamu wetu kwani pia tunatoa ushauri wa kitaalamu bure kulingana na ufaulu wa mwanafunzi na ni fani zipi ambazo anaweza kuomba ndani ya chuo chetu,” amesema Rose.

Rose amewahimiza wahitimu wa kidato cha nne, cha sita na kuendelea kwa ajili ya kufika kwenye banda hilo ili kujua ni kwa namna gani ya kujiendeleza huku akiwahimiza pia wawekezaji.

“Mbali na wanafunzi, pia tunawakaribisha wahitimu wa degrii kufika kwenye banda letu kwani elimu haina mwisho na kuona ni kwa namna gani wanaweza kujiendeleza.

“Pia hii ni fursa kwa wadau wetu waliosoma katika chuo chetu cha Mzumbe kufika kwa ajili ya kuona mambo mbalimbali yanayotekelezwa na chuo na kuona ni kwa namna gani nao wanaweza kutoa mchango wao katika kuboresha chuo chetu.

“Sambamba na hilo tunawakaribisha wawekezaji katika sekta mbalimbali kufika kwenye banda letu ili kujifunza sera ya uwekezaji na kuona ni namna gani wanaweza kushirkiana na chuo kwenye sekta hiyo, hivyo tunawakaribisha waje ili tuweze kujadiliana,” amesema Rose.

Maonyesho hayo ya Vyuo Vikuu ambayo yameanza Jumatatu ya Julai 18, yanatarajiwa kuhitimishwa Julai 22, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles