23.9 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

CHUO KIKUU CHA KIISLAMU CHAGEUKIA SERA YA VIWANDA

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM          |

CHUO Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM), kimejipanga kuiunga mkono Serikali ya Rais Dk. John Magufuli katika sera yake ya viwanda kwa kuimarisha na kuboresha vitivo vyake vya kitaaluma ili kujenga Tanzania ya viwanda.

MUM ni miongoni mwa vyuo vikuu 68 vinavyoshiriki maonyesho ya vyuo vya elimu ya juu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanayofanyika Dar es Salaam. Huu ni mwaka wake wa 13 kuonyesha shughuli mbalimbali za kitaaluma inazozifanya.

Kutokana na ubora wa elimu unaotolewa na chuo hicho, wananchi wengi waliojitokeza kwenye maonyesho hayo walivutiwa na umahiri wa ufundishaji wa lugha mbalimbali za kigeni kikiwamo Kichina, Kifaransa, Kiarabu na Kiingereza.

Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho (Taaluma), Dk. Abdallah Tego, alisema maonyesho hayo ya kila mwaka yamekuwa yakiwasaidia kuonyesha jinsi wanavyoisaidia Serikali na jamii kwa ujumla katika kukuza uchumi wa viwanda.

“Kuijenga Tanzania ya viwanda kunahitaji kuwepo na vyuo vitakavyozalisha wasomi weledi na wenye maadili, ambao watakuwa tayari kufanya kazi kwa masilahi mapana ya taifa letu.

“Nchi inaweza kuwa na wasomi wengi wenye maarifa na viwanda vikawepo, lakini kwa kukosa maadili, badala ya kulisaidia taifa, wanakuwa chanzo cha kukithitiri kwa mikataba mibovu na ongezeko la rushwa na vitendo vya ufisadi,” alisema Dk. Tego.

Kuhusu kozi za shahada mwaka huu, Dk. Tego alisema MUM inatarajia kudahili wanafunzi wa Bachelor of Low With Shariah, Business Studies, Arts & Humanities and Bachelor of Arts With Education.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,298FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles