25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chazindua ufadhili kwa wanafunzi

Brighiter Masaki

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimezindua ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kidato cha sita ambao wamepata viwango vya juu vya ufaulu katika masomo yao ya sayansi.

Akizindua ufadhili huo leo Februari 24, 2021 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekonolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema anakishukuru chuo hicho kwa kuanzisha jambo hilo ambalo linakwenda kuwa mkombozi kwa wanafunzi wanaotaka kuendelea na elimu ya juu lakini wanashindwa kutokana na changamoto mbalimbali.

Amesema anawaomba wanafunzi wote hasa wale wa kidato cha sita waliopo shuleni kusoma kwa bidi ili waweze kuwa miongoni mwa wanufaika wa ufadhili huo unaotolewa na chuo hicho.

“Sisi kama wizara tunatambua kazi kubwa inayofanywa na UDSM na tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha jambo hilo walilolianzisha linapata mafanikio makubwa, ila niwaondoe wasiwasi kuwa atutawaingilia katika upatikanaji wa wanafunzi hao.

“Tunahitaji kupata wataalamu watakaoweza kushindana vizuri katika soko la ajira na kusukuma gurudumu la maendeleo mbele, hivyo ufadhili huu utatusaidia kama nchi kupata wataalamu wengi” amesema Prof. Ndalichako

Hata hivyo amesema ufadhili huo ni fursa adimu kwa wanafunzi wanaotaka kujiendeleza zaidi kimasomo na kuongeza kuwa watamfatilia kila mwanafunzi atakayebahatika kuchaguliwa katika ufadhili huo.

Aidha Prof. Ndalichako amewataka wanafunzi hasa wa vyuo vikuu kutumia vizuri uhuru wanaoupata wanapokuwa vyuoni kwa kusoma tu na kuacha kufanya mambo yasiyofaha katika jamii.

“Mambo mengine kama starehe wanangu mtavikuta pindi utakapomaliza masomo, hakikisheni mnapokuwa chuoni mnafanya kile kilichowapeleka,” amesema

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo amesema kuwa upatikanaji wa wanufaika wa ufadhili huo utakuwa wa wazi hivyo amewataka wanafunzi hasa wa kidato cha sita kusoma kwa bidii ili waweze kuwa miongoni mwa watakochakuliwa kufadhiliwa na UDSM.

Naye Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye amesema kuwa walengwa wakubwa katika ufadhili huo ni watoto wa wakulima na wafanyakazi waliomaliza kidato cha sita na kupata daraja la juu la ufahulu katika masomo yao ya sayansi.

Amesema ili mwanafunzi aendelee kunufaika na ufadhili huo lazima aendelee kufanya vizuri kila mwaka katika masomo yake yote ya chuoni hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles