32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Chuo cha Malya chawanoa watunza viwanja vya michezo

Msigwa akiri hali ni mbaya 

Na Winfrida Mtoi,Mtanzania Digital

Chuo cha Maendeleo ya  Michezo Malya, kinaendesha mafunzo ya siku tano kwa wasimamizi wa viwanja  na wadau wengine wa michezo yenye lengo la kuwapa elimu ya utunzaji wa miundombinu viwanjani. 

Mafunzo hayo yamezinduliwa rasmi leo Novemba 29,2022  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, kwenye ukumbi wa Uwanja wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Msigwa amesema hali ya miundombinu ya michezo nchini ni mbaya  kutokana na ubora usioridhisha wa viwanja hasa mikoani.

Amewataka washiriki wa mafunzo hayo wakatengeneze mtizamo kwa jamii jinsi ya kujali miundombinu ya michezo na viwanja vitengenzwe kwa viwango.

“Ukija kuangalia viwango  vinavyoangaliwa hapa kwa Mkapa, sisi viwanja tulivyonavyo mikoani ni  mashamba ya nyasi. Mkitoka hapa kakaeni na mamlaka zetu muwaeleze. Kiwanja kina utaratibu wake wa kukitunza,” amesema Msigwa.

Aidha ameupongeza uongozi chuo hicho kwa kuandaa kozi hiyo, akiamini italeta mtizamo chanya wa utunzaji na utengenezaji wa miundombinu ya michezo badala ya kuachia Serikali pekee.

Naye Mkuu wa Chuo cha Malya, Richard Mganga, amesema ni mara ya kwanza wanaendesha kozi ya aina hiyo baada ya kubaini mameneja na wasimamizi wa viwanja vya michezo wanahitaji mafunzo ili kuboresha utendaji wao.

“Kwa muda mrefu hatujawakumbuka wasimamizi wa viwanja, tumebaini kuna pengo.Tumekuja na kozi hii kwa maana tunahitaji kuwa na watu wenye elimu ya utunzaji wa miundombinu ya viwanja vya michezo.

,Serikali inahimiza utunzaji wa viwanja lakini namna ya kuvitunza lazima tuwape elimu wadau wetu elimu,” amesema Mganga.

Meneja wa Uwanja wa Mkwakwani Tanga, Nassoro Makau  ni mmoja wa washiriki wa kozi hiyo, amesema  amejifunza mambo mengi mapya   ambayo ataweza kuwaelekeza wasaidizi wake jinsi ya kutunza vizuri uwanja huo.

Kwa upande wake, Issa Chiwile kutoka Bodi ya Ligi Zanzibar, ameeleza kuwa soka kwa sasa ni sayansi hivyo ni muhimu kupata elimu ili kuboresha utendaji kazi ukizingatia yeye ni mwandishi wa habari.

Mafunzo hayo yaliyoanza Jumatatu yakiwa na washiriki 53 yanatarajia kufikia tamati Jumamosi Desemba 2, 2023. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles