30.2 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Christian Bella kumsindikiza Miss Albino Novemba 27

Christian BellaNA GEORGE KAYALA

MFALME wa Sauti, Christian Bella, anatarajiwa kutumbuiza katika shindano la kumsaka mrembo albino ‘Miss Albino’ linalotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu, kwenye Ukumbi wa Msasani Club, jijini Dar es Salaam.

Shindano hilo awali lilipangwa kufanyika Septemba 4 mwaka huu katika Hoteli ya Serena, lakini likashindikana hadi lilipotangazwa tena.

Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la Save Vulnerable Foundation (SVF), Fredy Kaula, walioandaaa shindano hilo, alisema shughuli hiyo inalenga kuibua, kutambua vipaji, kujenga ujasiri na kuwawezesha kufikia malengo yao pamoja na kuwajenga kiafya, kiuchumi na kielimu.

Kiula aliongeza kwamba katika shindano hilo wanatarajia kukusanya Sh milioni 90 ili zisaidie ujenzi wa maktaba na jiko katika kituo cha walemavu kilichopo Buhangija, mkoani Shinyanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles