25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Christian Bella hana noma na Bongo Fleva

Glory Mlay – Dar es salaam

BOSI wa bendi ya Malaika, Christian Bella, amesema hana noma na muziki wa Bongo Fleva ndiyo maana huwasikiliza wasanii mbalimbali wanaofanya vizuri ili kupata maarifa mapya.

Bella ambaye yupo nchini Marekani kwenye ziara yake, ameliambia MTANZANIA kuwa huwa anasikiliza nyimbo za wasanii wa Bongo Fleva na anapogundua kuna makosa huwa anawafuata na kuwapa ushauri.

“Huwa nasikiliza kila wimbo wa msanii ambaye ameimba vizuri ila kwa nje namsikiliza sana Chris Brown kwa sababu hata majina yetu yanaendana yeye ni CB na mimi ni CBO.

“Wakati mwingine namsikiliza Diamond, Alikiba, Neddy Music na wengine wengi,” alisema Bella.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles