23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Chris Brown atarajia mtoto wa pili

LOS ANGELES, MAREKANI

STAA wa muziki wa RnB, Chris Brown, ameripotiwa kuwa, anatarajia mtoto wa pili na aliyekuwa mpenzi wake Ammika Harris.

Kwa mujibu wa Page Six, msanii huyo mwenye umri wa miaka 30, ameachana na mpenzi wake wa sasa Indyamarie Jean Pelton baada ya kupata taarifa kwamba Chris amempa ujauzito mpenzi wake wa zamani Ammika.

Mara ya mwisho msanii huyo kuonekana na mrembo huyo ambaye amempa ujauzito ilikuwa Januari mwaka huu huko nchini Ufaransa na ndipo akampa ujauzito huo.

Chris kwa sasa ana mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka mitano akijulikana kwa jina la Royalty. Mtoto huyo alikuja kujulikana huku akiwa na umri wa miezi tisa na mama yake ni Nia Guzman raia wa nchini Brazil.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles