27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Chris Brown ampotezea Rihanna

NEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, ameonekana kumpotezea mpenzi wake wa zamani Rihanna baada ya kushindwa kumtakia heri siku yake ya kuzaliwa.

Februari 20, Rihanna alikuwa anasherehekea kumbukizi ya kuzaliwa kwake huku akiwa anatimiza miaka 32. Kwa kawaida Chris Brown amekuwa akimtakia heri kila ifikapo siku kama hiyo.

Wawili hao walikuwa wapenzi kwa kipindi kirefu, lakini wakaja kuachana mwaka 2013, baada ya hapo Chris akafanikiwa kupata mtoto wa kwanza anayejulikana kwa jina la Royality na Novemba mwaka jana akafanikiwa kupata mtoto mwingine Aeko.

Kwa mujibu wa mtandao wa Hollywood Life, Chris ameamua kumuweka pembeni Rihanna huku muda mwingi akiutumia kuwaangalia watoto wake, hivyo hata mitandao ya kijamii haonekani mara kwa mara.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles