23.5 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Chris Brown amchokoza mpenzi wa Karrueche Tran

MIAMI, MAREKANI 

CHRIS Brown amelianzisha bifu jipya na mpenzi wa Karrueche Tran ambaye anajulikana kwa jina la Victor Cruz kwa madai kuwa hajui kuvaa vizuri.

Chris aliwahi kuwa kwenye uhusiano na Karrueche, lakini baada ya kuachana mrembo huyo akajikuta anaingia kwenye uhusiano na nyota huyo wa mchezo wa soka wa Marekani.

Mwishoni mwa wiki iliopita mjini Miami ilikuwa ni wiki ya wanaume kupendeza, hivyo Karrueche na mpenzi wake huyo waliposti picha kwenye mitandao ya kijamii ambazo zilikuwa zinawaonesha wakiwa mitaani.

Chris alishindwa kuzuia hisia zake na kuamua kutoa somo kwa mpenzi wake huyo wa zamani jinsi ya kuwafanya wapendeze.

“Hakuna kitu kibaya ambacho ninaweza kukifanya, lakini kitu ambacho ninaweza kukisema ni kwamba Karrueche unatakiwa kuhakikisha huyo jamaa anapendeza, nguo alizovaa sijui alinunua wapi, inaonekana hana watu wazuri wa kumfanya apendeze akiwa anaenda kununua nguo, anaonekana anavaa kizamani,” aliandika Chris.

Hata hivyo, wawili hao wameonekana kuwa na busara kwa kuwa hadi sasa wamekaa kimya hawakutaka kujibu ujumbe huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles