Chris Brown ambeba Davido

0
1164

NEW YORK, MAREKANI

STAA wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, anazidi kumbeba mkali wa muziki nchini Nigerian, Davido baada ya kupanda naye kwenye jukwaa moja huko jijini New York.

Kwa sasa Chris Brown yupo kwenye ziara hiyo ya muziki, hivyo aliamua kumpa nafasi Davido ili aonesha umahili wake baada ya kufanya naye kazi ya wimbo mmoja ambao waliuachia mwezi uliopita.

Baada ya Davido kupewa nafasi hiyo hakujiacha nyuma aliwapagawisha mashabiki zake baada ya kuimba nyimbo mbili ambazo zilizidi kumpa jina kubwa kwenye muziki. Nyimbo hizo ni IF, FALL na kisha wakaimba wimbo wao wa pamoja Blow My Mind.

Hata hivyo kuna taarifa kwamba Davido ataendelea na ziara hiyo na Chris Brown kwa miji sita nchini Marekani, hivyo ni sehemu ya Davido kuutangaza muziki wa Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here