NEW YORK, MAREKANI
MKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, amedai kuwa kuna watu wanaouza habari zake za kila siku kwenye mtandao wa TMZ.
Brown amesema anashangaa kuona baadhi ya mambo yake anayoyafanya kila siku lazima wayapate TMZ, hivyo anaamini kuna watu ambao wanapiga pesa kupitia habari zake.
TMZ ni tovuti ambayo inaelezea habari mbalimbali za watu maarufu, mtandao huo ulianzishwa Novemba 8, mwaka 2005 na kazi yao kubwa ni kununua stori na kuzisambaza.
“Kuna watu wanaofuatilia maisha yangu kuanzia naamka nadi nalala, baadhi ya mambo ambayo ninayafanya kila siku nayaona TMZ, ninaamini kuna watu wanauza habari zangu, maisha yao yanakwenda sawa kwa ajili yangu, ipo siku nitawanasa,” alisema Chris.