28.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Chongolo aitaka Wizara ya Ardhi kupima maeneo ya huduma

Na Safina Sarwatt, Rombo

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ametoa maelekezo kwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupima maeneo ya huduma na kutambua mipaka sambamba na kutoa hati miliki ili yamilikiwe kisheria.

Chongolo ametoa maelekezo hayo leo Agosti 5, 2022 wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro baada ya kukagua ujenzi sekondari ya Mamsera.

Amesema maeneo yote ya huduma ni lazima sasa yakapimwe na mipaka yake katambuliwa na kupatiwa hati ili kudhibithi tatizo la uvamizi wa maeneo hayo.

“Lazima tujenge tamaduni za kupima kuwa na hati miliki maeneo yote ya umma ikiwemo shule, hospitali na maeneo ya wazi tusipofanya hivyo tutakosa maeneo ya huduma,” amesema Chongolo.

Amesema maeneo yote ya huduma lazima yamilikiwe kisheria ili kuepukana na migogoro na uvamizi.

“Naelekeza Wizara ya Ardhi iweke program za kuyatambua meaneo hayo ya huduma ndani ya miaka mikatano wawe wamemaliza kuyapima na kutoa hati miliki mwasababu wajaja ni wengi watavamia maeneo hayo.

“Tunafanya hivyo ili tujihakikishie uhakika wa umiliki na mtambue mipaka yenu, tunzeni nyaraka zenu,” amesema Chongolo.

Katika hatua nyingine Chongolo amesema kuwa Serikali inawajibu wa kuwahudumia wananchi hivyo ni vema sasa wahusika wakatekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi amesema Rais Samia Suluhu ametoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya Rombo.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema watasimamia miradi yote inayotekelezwa na serikali ili ijengwe katika viwango vinavyotakiwa kulingana na thamani ya fedha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles