23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Chongolo ahimiza ujenzi wa Kiwanda cha nguo Simiyu

Na Derick Milton, Simiyu

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo pamoja na mambo mengine ameitaka Serikali kuanza ujenzi wa viwanda vya nguo katika Mkoa wa Simiyu na maeneo mengine ambapo zao la pamba linalimwa kwa wingi.

Katibu Mkuu ameyasema hayo Jumatatu Januari 31, 2022 katika ziara maalum ya Sekretarieti ya HKT katika mkoa wa Simiyu yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuhimiza uhai wa chama ngazi ya mashina.

“Ni lazima mtengeneze mazingira yakuwa na pamba inayoanzia hapa na kuvaliwa hapa. Kiwanda kijengwe hapa Bariadi na pamba ichakatwe hapa ili matokea yaonekane hapa, lazima tuweke msukumo viwanda vijengwe hapa, na nguo zinazotokana na pamba yetu kwa sababu ni bora na nguo zitakuwa bora,” amesema Chongolo.

Katibu Mkuu ameyasema hayo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila akieleza mafanikio makubwa wanayotarajia kuyapata katika uzalishaji wa zao hilo la Pamba mwaka huu.

Aidha katika hatua nyingine, Katibu Mkuu ametembelea na kukagua mashamba ya wakulima wa pamba katika wilaya ya Bariadi, maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za CCM za Matawi na Kata, ujenzi wa Barabara ya Somanda – Isakalyamhela pamoja na Kuhudhuria mkutano wa shina namba 8 kata ya Nkololo.

Katika ziara hiyo Wilayani Bariadi, Katibu Mkuu ameambatana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shamsa Mohammed Seifu pamoja na Mkuu wa Mkoa huo, David Kafulila.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles