33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Chirwa, Azam FC bado hakijaeleweka

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

LICHA ya kuwaongezea mikataba mipya baadhi ya wachezaji wao, uongozi wa klabu ya Azam FC hadi sasa bado haujafanya mazungumzo na mshambuliaji wao mahiri raia wa Zambia,  Obrey Chirwa.

Tayari Azam imerefusha mikataba mipya ya wachezaji Donald Ngoma, Yakubu Mohamed, Bruce Kangwa, Salmin Hoza na Mwadini Ally.

Lakini haujaafikiana na Chirwa ambaye ni mkataba wake wa mwaka mmoja umekwisha, baada ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita kufikia tamati.


Akizungumza na MTANZANIA jana, Mratibu wa timu hiyo, Philipho Alando, alisema mchezaji huyo kwa sasa yupo  mapumzikoni nchini kwao, lakini hawajaafikiana nae kuhusu kuendelea kuichezea timu yao.

“Siwezi kusema kuwa tumeshaanza mazungumzo na Chirwa au bado ila hadi sasa hajaongeza mkataba kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa sasa yupo mapumzikoni kwao,” alisema.

Akizungumzia kambi ya kujiandaa na michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu Kombe la Kagame ambayo itatimua vumbi Julai 7 hadi 21 mwaka huu nchini Rwanda, alisema wanatarajia kuanza maandalizi Juni 20 mwaka huu.

Wakati huo huo, klabu hiyo kesho itamtambulisha rasmi kocha wao mpya, Ettiene Ndayiragije.

Ndayiragije ameafikiana kuifundisha Azam, baada ya msimu uliopita kuinoa KMC ya Kinondoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles